Kuna mbinu za mpangilio wa Tor Browser kama browser yako, lakini njia zote zinaweza zisifanye kazi kila mara au kwa kila mfumo wa uendeshaji. Tor Browser inafanya kazi kwa bidii kujitenga yenyewe katika mfumo wako, na hatua za kuifanya mfumo wa browser usipatikane. Hii humaanisha muda mwingine tovuti inaweza ikazunguka katika Tor Browser, na muda mwingine itazunguka katika browser nyingine. Aina hii ya tabia inaweza kuwa hatari na kuvunja kutojulikana.