Ikiwa upatikaji wako wa mtandao haujadhibitiwa, unapaswa kuzingatia kusanikisha na kuboresha Snowflake ili kuwasaidia watumiaji katika udhibiti wa mtandao. Wakati unaitumia Snowflake katika shughuli mbalimbali za browser, utatoa muunganisho kama proxy kwa entry node katika mtandao wa Tor, na ndio hivyo tu.

Ongeza-katika

Kwanza hakikisha unawezesha WebRTC. Halafu unaweza kusanikisha hii addon for Firefox au add-on for Chrome ambayo itakufanya wewe kuwa Snowflake proxy. Pia inaweza kukutaarifu kuhusu watu wangapi uliwasaidi katika masaa 24 yaliyopita.

Kurasa ya tovuti

Katika browser ambapo WebRTC imewezeshwa: Kama hutaki kuongeza Snowflake katika browser yako, unaweza kuingia katika https://snowflake.torproject.org/embed na ugeuze kitufe ili kuchagua kuingia kuwa proxy. Huwezi kufunga kurasa kama unataka kubakiza Snowflake proxy.