Wahalifu wanaweza kufanya vitu vibaya. Kwa kuwa wamedhamiria kuvunja sheria, na wana machaguzi mengi ambayo hutoa faragha bora zaidi ya inavyotoa Tor. Wanaweza kuiba simu ya mkononi, kuitumia, na kuitupa shimoni; Wanaweza kuharibu mifumo ya kompyuta nchini Korea au Brazil na kuitumia kuanzisha shughuli za unyanyasaji; Wanaweza kutumia programu hatarishi, programu haribifu, na mbinu zingine kufanya udhibiti wa mamilioni windows za kompyuta dunia kote.

Lengo la Tor ni kuwapatia ulinzi kwa watu wa kawaida wanaotaka kufuata sheria. Wahalifu pekee wana faragha kwa sasa, na tunatakiwa kurekebisha hilo.

Baadhi ya watetezi wasiojulikana hueleza hii ni biashara tu — kukubali matumizi mabaya kwa mazuri — lakini kuna zaidi ya hayo. Wahalifu na watu wengine wabaya wanahamasika kujifunza namna ya kutojulikana vizuri na wengi huhamasika zaidi kulipa vizuri ili kufanikisha hilo. Kuwa na uwezo wa kuiba na kutumia tena vitambulisho vya waarika wasio na hatia (utambulisho wa wizi) hurahisisha zaidi. Watu wa kawaida, kwa upande mwingine, hawana muda au pesa kufagamu namna ya kupata faragha online. Hii ni mbaya zaidi inayowezekana duniani mwote.

Hivyo ni kweli, wahalifu wanaweza kutumia Tor, lakini wana machaua bora zaidi, na inaonekana haiwezekani kuondosha Tor kwenye ulimwengu itawazuia kufanya vitu vyao vibaya. Wakati huo huo, Tor na vipimo vingine vya faragha inaweza kupambana na wizi wa uthibitisho, uhalifu wa kimwili kama kuvizia, na kadhalika.